• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Russia yailaani Marekani kwa kuharibu mfumo wa udhibiti wa silaha

    (GMT+08:00) 2019-02-10 16:41:04

    Balozi wa kudumu wa Russia kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Vasily Nebenzya jana alisema, Marekani inaharibu mfumo wa udhibiti wa silaha duniani, na kutaka kuongeza akiba ya silaha zake, vitendo ambavyo vinatishia usalama wa dunia, pia huenda vikasababisha matokeo mabaya yasiyoweza kutarajiwa.

    Balozi Nebenzya amesema, Russia haiwezi kutarajia maendeleo ya hali hiyo katika siku za baadaye, na hatari ya kutokea kwa mgogoro inaongezeka.

    Wizara ya mambo ya nje ya Marekani tarehe 1 mwezi huu ilitangaza kuzindua utaratibu wa kujitoa kwenye Mkataba wa makombora ya masafa ya kati INF kuanzia tarehe 2 mwezi huu. Rais Vladimir Putin wa Russia pia alitangaza kusitisha mkabata wa INF, na kusema hatatangaza kufanya mazungumzo mapya ya kimataifa kuhusu mkataba huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako