• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SADC yazishutumu nchi zinazodhoofisha serikali ya Venezuela inayoongozwa na rais Maduro

    (GMT+08:00) 2019-02-11 08:56:26

    Rais wa Namibia na mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC Hage Geingob amezishutumu nchi zinazolenga kuingilia kati masuala ya ndani na mamlaka ya Jamhuri ya Venezuela. Ametoa taarifa akisema nchi hizo zinajaribu kudhoofisha serikali ya Venezuela iliyochaguliwa kidemokrasia na kuongozwa na rais Nocolas Maduro Moros, kwa kumtangaza Juan Guaido Marquez kuwa rais wa muda wa nchi hiyo. Amesema SADC inapinga vitendo vya kukiuka kanuni za sheria ya kimataifa, ikiwemo kuheshimu mamlaka na kutoingilia kati masuala ya ndani ya mataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako