• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bw. Guterres ataja amani na usalama na mabadiliko ya hali ya hewa kama changamoto kuu za Afrika

    (GMT+08:00) 2019-02-11 08:57:44

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres jana alitaja amani na usalama pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa kuwa ni changamoto mbili kuu zinazoikabili Afrika kwa hivi sasa.

    Bw. Guterres ameyasema hayo wakati akihutubia ufunguzi wa mkutano wa kilele wa 32 wa Umoja wa Afrika unaofanyika kwa siku mbili kuanzia Februari 10 na kumalizika Februari 11 katika makao makuu ya umoja huo Addis Ababa nchini Ethiopia. Kulingana na Bw. Guterres juhudi za Umoja wa Afrika za kuondoa mapambano hadi kufikia 2020 zinaendelea kuzaa matunda akitolea mfano wa Ethiopia na Eritrea ambazo zimesaini makubaliano ya kihistoria ya amani. Amesema Umoja wa Mataifa unaendelea kuunga mkono operesheni za amani za Afrika na kusisitiza kwamba hivi karibuni wamezindua Mpango wa kuchukua Hatua za Amani ambao unawezesha tume kufanya kazi kwa ufanisi, kuwa na vifaa bora, salama na imara zaidi.

    Mbali na hayo Bw. Guterres amesema mabadiliko ya hali ya hewa ni changamoto kubwa zaidi ambayo bado inaendelea kukua kwa kasi kuliko juhudi zinazochukuliwa za kuzipunguza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako