• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika apongeza ushirikiano wa AU na China

    (GMT+08:00) 2019-02-11 08:58:06

    Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat, amepongeza ushirikiano kati ya nchi wanachama wa Umoja wa Afrika na China katika maeneo mbalimbali.

    Bw. Mahamat, ametoa pongezi hizo jana kwenye ufunguzi wa mkutano wa kilele wa 32 wa Umoja wa Afrika huko Addis Ababa Ethiopia, ambao unahudhuriwa na viongozi wa Afrika, wanadiplomasia wa kigeni, na watu wengine maarufu. Akiongelea kuhusu ushirikiano kati ya China na Afrika Bw. Mahamat amesema pande mbili zinaendelea kufurahia ushirikiano wenye nguvu kubwa.

    Amesema baada ya mkutano wa FOCAC uliofanyika kwa mafanikio Septemba 2018, Umoja wa Afrika ulizindua rasmi ofisi ya uwakilishi hapa Beijing, na kusisitiza kuwa ofisi hiyo itaimarisha zaidi ushirikiano unaozaa matunda, ikiwa ni pamoja na kufanya mazungumzo ya kimkakati kati ya Kamisheni ya Umoja wa Afrika na Jamhuri ya watu wa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako