• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yasema itawabakisha washauri wake nchini Iraq na Syria

    (GMT+08:00) 2019-02-11 09:27:48

    Mnadhimu mkuu wa jeshi la Iran Meja Jenerali Mohammad Baqeri jana alisema Iran itawabakisha washauri wa kijeshi nchini Iraq na Syria kama nchi hizo zinahitaji.

    Shirika la habari la Iran IRNA limemnukuu Baqeri akisema kuwa Iran imezipatia Syria na Iraq msaada wa ushauri kwa ajili ya kupambana na tishio la ugaidi, pia itawatumikia watu wa nchi hizo kulingana na mahitaji yao.

    Baqeri amesema madhali nchi hizo zinataka, Iran itaendelea kuwaweka washauri wake, na itawaondoa wakati wowote watakapokuwa hawataki, kinyume na wanajeshi wa Marekani ambao wapo katika nchi hizo bila nchi hizo kutaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako