• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Israel yayataja mauaji ya mwanamke wa Israel kama shambulizi la kigaidi

    (GMT+08:00) 2019-02-11 09:28:05

    Idara ya usalama ya Israel Shin Bet jana ilisema mauaji ya mwanamke wa Israel Ori Ansbaher mwenye umri wa miaka 19 wiki iliyopita ni "shambulizi la kigaidi" lililofanywa na mwanamume wa Palestina.

    Idara ya Shin Bet imesema mahojiano ya Arafat Irfayia mwenye umri wa miaka 29 ambaye alikamatwa Ijumaa wiki iliyopita mjini Ramallah kwenye Ukingo wa Magharibi, yanaonesha mauaji hayo yalitokana na itikadi ya utaifa.

    Habari nyingine zinasema, Israel inapanga kuzuia baadhi ya fedha zinazohamishwa na Israel kwa serikali ya Palestina kila mwezi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako