• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: FIFA yachunguza ripoti ya kuwepo kwa njama za kushindwa kwa Harambee Stars

    (GMT+08:00) 2019-02-11 10:46:06

    Shirikisho la soka duniani (FIFA), limethibitisha kuwa linachunguza ripoti ya kuwepo kwa matukio ya kupanga mechi ya timu ya taifa ya soka ya Kenya Harambee Stars, katika miaka iliyopita.

    Hatua hii ya FIFA imekuja baada ya ripoti ya uchunguzi ya gazeti la kila siku nchini humo la Daily Nation, kuripoti kuwa beki wa zamani George Owino alihusika na kosa hilo kati ya mwaka 2009 mwezi Juni hadi mwezi Machi mwaka 2011.

    Inadaiwa kuwa mchezaji huyo na wengine watatu ambao hawajatambuliwa walilipwa mamilioni ya fedha za Kenya na rais wa Singapore, Raj Perumal ili kusababisha Harambee Stars kushindwa wakati wa michuano ya kimataifa.

    Kanuni za FIFA zinaeleza kuwa, mchezaji au yeyote anayebainika kuwa alihusika na kosa la upangaji wa matokeo, ataadhibiwa kwa faini ya Dola 100,000 na kufungiwa kutoshiriki katika masuala ya soka kwa angalau miaka mitano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako