• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Fainali za kufuzu kombe la dunia kwa wachezaji wa umri wa chini ya miaka 20- Senegal yawa ya kwanza kufuzu

    (GMT+08:00) 2019-02-11 10:46:45

    Timu ya taifa ya Senegal ya vijana wasiozidi miaka 20 (Young Lions of Teranga) imekuwa ya kwanza kufuzu katika fainali ya kombe la Dunia itakapigwa mwezi Mei nchini Poland.

    Hii imekuja baada ya timu hiyo kuishinda Ghana mabao 2-0 katika mechi ya pili, kuwania ubingwa wa Afrika, mashindano yanayoendelea nchini Niger.

    Senegal wanaongoza kundi la B kwa alama sita, baada ya kucheza mechi ya kwanza dhidi ya Mali pia kwa mabao 2-0.

    Mataifa mengine yaliyofuzu kwingineko duniani ni pamoja na:-

    Barani Asia: Japan, Korea, Qatar na Saudi Arabia

    Bara la Amerika, Concacaf: Honduras, Mexico, Panama na Marekani.

    Eneo la Visiwa na Bahari: New Zealand and Tahiti

    Barani Ulaya: Ufaransa, Italia, Norway, Ureno na Ukraine

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako