• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • NDONDI: Mganda achakazwa raundi ya kumi

    (GMT+08:00) 2019-02-11 10:47:05

    Bondia wa Uganda Sharif Bogere ajulikanaye zaidi kama Simba amepoteza mchezo wake dhidi ya Javier Fortuna wa Jamhuri ya Domonica katika raundi ya 10 ya pambano lao lililopigwa kwenye ukumbi wa michezo wa Carson jijini California Marekani wikiendi iliyopita.

    Majaji wote watatu kwa pamoja walitoa alama za 96-93 kwa Javier Fortuna. Katika raundi ya 6, Bogere alionekana kuumudu mchezo kwa kumshushia ngumi za kutosha mpinzani wake, lakini kuanzia raundi ya 7 kibao kilibadilika na kujikuta akikung'utwa mfululizo hadi katika raundi hiyo ya 10 mwamuzi alipomnusuru kwa kumaliza pambano na waamuzi kumpa ushindi Javier.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako