• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yaadhimisha miaka 40 ya kumbukumbu ya Mapinduzi ya Kiislam

    (GMT+08:00) 2019-02-11 17:02:46

    Maelfu ya Wairan wameshiriki katika maandamano yaliyofanyika nchi nzima kusherehekea kumbukumbu ya miaka 40 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislam.

    Katika mji mkuu wa nchi hiyo, Tehran, watu walijaa barabarani huku wakibeba mabango yenye maneno yanayopinga Marekani na Israel, na kubeba picha za aliyekuwa mwanzilishi wa nchi hiyo ya kiislam, Ayatollah Ruhollah Khomeini, na mrithi wake na kiongozi wa ngazi ya juu wa sasa wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei.

    Khamenei amelaani hatua za uchochezi zinazofanywa na Marekani dhidi ya Iran, na kutaka watu wajitokeze kwa wingi kuadhimisha siku hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako