• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Uganda na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa wajadili suala la usalama wa kikanda

    (GMT+08:00) 2019-02-11 17:22:15

    Rais Yoweri Museveni wa Uganda jana amekutana na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres pamoja na maofisa kadhaa wa Umoja huo, na kujadili suala la usalama wa kikanda, kando ya mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika unaofanyika huko Addis Ababa, Ethiopia.

    Taarifa iliyotolewa na serikali ya Uganda imesema, Bw. Guterres amesema atafanya juhudi kuhamasisha rasilimali ili kuunga mkono ujumbe wa Umoja wa Mataifa barani Afrika, na kuimarisha mamlaka yake kutoka ulinzi wa amani hadi utekelezaji wa operesheni.

    Rais Museveni amesema, nchi za Afrika lazima zijenge majeshi yenye mtazamo sahihi ili kuepusha migogoro inayoendelea barani humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako