• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matumizi ya fedha ya wananchi wa China yapata maendeleo makubwa wakati wa Sikukuu ya Spring

  (GMT+08:00) 2019-02-11 18:50:50

  Takwimu mbalimbali kuhusu mapumziko ya sikukuu ya Spring zimetolewa leo.

  Takwimu hizo zinaonyesha thamani ya mauzo ya kampuni za bidhaa za rejareja na vyakula nchini China ambayo imezidi dola za kimarekani bilioni 149.3, ikiwa ni ongezeko la asilimia 8.5 kuliko mwaka jana wakati kama huo. Pia idadi ya watalii imefikia milioni 415, ikiwa ni ongezeko la asilimia 7.6, huku pato linalotokana na utalii likifikia dola za kimarekani bilioni 76.7, ikiwa ni ongezeko la asilimia 8.2.

  Wakati uchumi wa dunia unapokabiliwa na changamoto za kujilinda kibiashara na hali ya wasiwasi, soko la matumizi ya fedha wakati wa Sikukuu ya Spring ya China limepata maendeleo mazuri, ikionesha mustakabali mzuri wa soko na uchumi wa China, pamoja na imani thabiti ya wananchi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako