• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia: Ethio Telecom kuuzwa kwa mwekezaji wa kibinafsi

    (GMT+08:00) 2019-02-11 18:57:54

    Serikali ya Ethiopia imechangua kampuni ya umma ya mawasiliano Ethio Telecom kuwa ya kwanza kuuzwa kwa mwekezaji wa kibinafsi.

    Tangu alipochukua hatamu za uongozi, waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ameanzisha sera kadhaa za kukuza uchumi wa nchi hiyo yenye zaidi ya watu miloni 100.

    Uuzazi au ubinafsishwaji wa mashirika ya serikali ni miongoni mwa mipango ya serikali ya kuendeleza uchumi.

    Uwekezaji wa kibinafsi umekabiliwa na ukosefu wa fedha za kigeni huku Ethiopia ikiwa kwenye nafasi ya 159 kati ya 190 zenye urahisi wa kufanya biashara.

    Waziri wa fedha nchini humo Haji Ebsa, amesema kamati za kiufundi zimeundwa ili kufanikisha uuzaji huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako