• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Wakulima walalamikia kupungua kwa bei ya maziwa

    (GMT+08:00) 2019-02-11 19:00:00

    Wenye viwanda vya maziwa nchini Kenya wamepunguza bei ya bidhaa hiyo kutoka kwa wafugaji kwa shilingi tatu.

    Halmasharui ya bidhaa za maziwa nchini humo imesema kumekuwa na ongezeko la maziwa na hivyo bei ya awali itamaanisha baadhi ya wakulima hawatauza maziwa yao.

    Hata hivyo kulingana na halmashauri hiyo bei ya bidhaa hiyo madukani haitapungua.

    Wakulima wamelalamikia hatua hiyo wakisema tayari wanakabiliwa na gharama ya juu ya uzalishaji kutokana na kupanda kwa bei ya pembejeo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako