• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Wajasiriamali Tanzania, wapewa elimu kuhusiana na taratibu za kupata leseni ya TBS

  (GMT+08:00) 2019-02-11 19:01:10

  Wajasiriamali wa nafaka, maziwa, rangi, asali na unga lishe nchini Tanzania, wamepatiwa elimu kuhusiana na taratibu za kufuata ili kupata leseni ya kutumia alama ya ubora ya TBS kutokana na huduma hiyo kuwa inatolewa bure kwa wajasiriamali.

  Ofisa Uhusiano wa TBS, Neema Mtemvu, amesema wajasiriamali walionyesha kufurahishwa na elimu waliyoipata na waliahidi kutuma maombi TBS na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), ili kuomba wataalamu wa nafaka kwenda kuwapa elimu juu ya madhara yatokanayo na upakaji mafuta kwenye michele na njia sahihi ya kuandaa nafaka zao.

  Mtemvu, alisema wamelenga wajasiriamali kwa kuwa ndilo kundi muhimu katika kukuza uchumi, hivyo alitoa wito kwao kutumia fursa zinazotolewa na shirika hilo kukuza thamani ya bidhaa zao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako