• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Tanzania yaanza uuzaji wa mahindi kwenda nchi zenye njaa

    (GMT+08:00) 2019-02-11 19:01:33

    Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) nchini Tanzania umeanza kusafirisha mahindi kwenda nchi zenye njaa tani 36,000 ikiwa ni sehemu ya mkataba baina yake na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula (WFP).

    Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFRA, Vumilia Zikankumba, amesema kuwa wameshasafirisha mahindi takribani tani 15,000 kwenda katika Uganda na Sudani Kusini.

    Alisema mkataba huo ambao uliingiwa kati ya NFRA na WFP ambao pia ulishuhudiwa na Rais John Magufuli, na katika awamu ya kwanza ya mkataba watasafirisha tani 36,000.

    Aidha, aliwataka wakulima kutumia fursa hiyo ya NFRA, kuuza mahindi nje ya nchi ili kulima kwa wingi na kuzingatia ubora.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako