• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Castle Lager yafungua bonge la fursa kwa wachezaji Afrika

  (GMT+08:00) 2019-02-12 08:12:20
  Mashindano ya Castle Lager 5 msimu wa pili yamezinduliwa rasmi jana nchini Afrika Kusini katika jiji la Johennesburg ambayo ni mashindano ya kabumbu yanayoshirikisha wachezaji watano watano.

  Msimu wa kwanza nchi 5 zilishiriki ambazo ni Zambia, Afrika Kusini, Tanzania, Eswatini na Zimbabwe na kushuhudia Afrika Kusini ikitwaa ubingwa huo katika fainali zilizofanyika Zambia. Mwaka huu Castle Lager 5 imeongeza washiriki kutoka watano hadi nane huku fainali zake zikitarajia kufanyika nchini Tanzania.

  Nchi zinazoshiriki ni wenyeji Tanzania, Uganda, Zambia, Afrika Kusini, Eswatini, Ghana, Nigeria na Zimbabwe, bingwa wa mwaka huu atapata fursa ya kwenda barani Ulaya ambapo nchi itatajwa baadaye.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako