• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afisa wa AU aishukuru China kwa kuunga mkono maendeleo ya ujenzi wa uwezo

    (GMT+08:00) 2019-02-12 08:44:14

    Katibu mtendaji wa Mfuko wa Kujenga Uwezo wa Afrika Emannuel Nnadozie ACBF, jana aliishauri China kuunga mkono zaidi juhudi za kujenga uwezo wa Afrika, akisema wameangalia na kuridhishwa na uungaji mkono katika nyanja mbalimbali unaotolewa na serikali ya China katika kujenga uwezo kwenye maeneo yanayohitajika.

    Akiongea na shirika la habari la China Xinhua, Nnadozie amesema wanafahamu udhamini wanaopewa vijana wa Afrika wa kusoma nchini China na baadaye kurudi Afrika kusaidia kukuza maendeleo.

    Kulingana na ubalozi wa China nchini Ethiopia hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2017, serikali ya China imewapatia mafunzo washiriki 5,655 wa Ethiopia kwenye taaluma mbalimbali zikiwemo za sekta za elimu, afya na huduma za matibabu, kilimo, utalii, viwanda vya utengenezaji, utawala wa umma, usimamizi wa biashara, maendeleo ya miji na kutokomeza umasikini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako