• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan yakanusha kuwepo kwa miili 300 katika hospitali

    (GMT+08:00) 2019-02-12 09:10:13

    Wizara ya afya ya jimbo la Khartoum la Sudan imekanusha kuwepo kwa miili 300 kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali moja mjini Khartoum.

    Wizara hiyo imesema kupitia taarifa kuwa, habari zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kuwepo kwa miili 300 ya watu wasiotambuliwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mafunzo mjini Khartoum, hazina msingi wowote, na kuonya kuwa kueneza habari za uvumi kama hizo bila kuzithibitisha kunalenga kuzusha hofu kwenye jamii.

    Baadhi ya wanaharakati walisema kwenye mitandao ya kijamii kuwa miili 300 ya watu wasiotambuliwa inahifadhiwa kwenye hospitali ya mafunzo mjini Khartoum, na hao wote ni wahanga wa maandamano makubwa yanayoendelea nchini Sudan.

    Kwa mujibu wa takwimu za serikali, mpaka sasa watu 31 wameuawa kwenye maandamano hayo tangu yalipoanza mwezi Desemba mwaka jana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako