• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Tanzania laimarisha juhudi za serikali za kutokomeza mauaji ya watoto

    (GMT+08:00) 2019-02-12 09:10:34

    Mkuu wa jeshi la Tanzania Jenerali Venance Mabeyo amesema jeshi la Tanzania limeimarisha juhudi za serikali zinazolenga kutokomeza mauaji ya kikatili dhidi ya watoto kwenye eneo la Njombe, kusini mwa nchi hiyo.

    Jenerali Mabeyo alifanya mazungumzo na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya eneo le Njombe kujadili njia za kukomesha mauaji hayo.

    Mazungumzo hayo pia yalihudhuriwa na wajumbe wa kikosi maalumu ambacho kimetumwa kwenye eneo hilo kuchunguza na kukamata wapangaji wa mauaji hayo yanayohusiana na imani za kishirikina.

    Jenerali Mabeyo amesema tangu habari kuhusu mauaji hayo ya kikatili dhidi ya watoto wasio na hatia ziliposambaa kote nchini Tanzania na nje ya nchi hiyo, zimezusha hofu kubwa kwa baadhi ya watanzania.

    Bw. Mabeyo ametoa wito kwa wakazi wa eneo la Njombe wawe watulivu wakati mamlaka husika zinachunguza chanzo cha mauaji hayo na kuwafikisha wahusika mbele ya vyombo vya sheria.

    Imefahamika kuwa watoto wasiopungua kumi wameuawa kwa njia ya kikatili kwenye eneo la Njombe ndani ya mwezi mmoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako