• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yakamata bidhaa feki zenye thamani ya dola milioni 85 za kimarekani ndani ya miezi sita

    (GMT+08:00) 2019-02-12 09:21:48

    Mwenyekiti wa shirika la kupambana na bidhaa feki ACA Bibi Flora Mutahi jana alisema Kenya imekamata bidhaa feki zenye thamani ya dola milioni 85 za kimarekani ndani ya miezi sita iliyopita.

    Mutahi amesema ingawa Kenya imeweka sheria za kuadhibu bidhaa feki, lakini bado inahitaji kufanya juhudi za kupambana na tishio linalotokana na bidhaa hizo.

    Akihutubia kongamano la vyombo vya habari nchini Kenya Mutahi amesema hatari ya kutengeneza bidhaa feki ni kubwa, kwa kuwa biashara haramu inatokea kwenye sehemu zinazokumbwa na ufisadi. Ameongeza kuwa Kenya inapata hasara yenye thamani ya dola bilioni 2 za kimarekani kila mwaka kutokana na biashara ya bidhaa feki, hususan simu za mkononi, pombe na vinywaji, DVD, CD, maji ya chupa na dawa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako