• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sudan Kusini yahimiza kuchunguza ajali ya kuanguka kwa helikopta ya walinzi wa amani

  (GMT+08:00) 2019-02-12 09:22:10

  Serikali ya Sudan Kusini jana imehimiza Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kufanya uchunguzi wa pamoja ulio wazi wa ajali ya kuanguka kwa helikopta ya kijeshi ya Ethiopia iliyotokea Jumamosi wiki iliyopita.

  Ajali hiyo ilitokea kwenye eneo la Abyei lililoko kati ya Sudan na Sudan Kusini, na kusababisha vifo vya wahudumu watatu wa ndege, na abiria wengine kumi wamejeruhiwa.

  Wizara ya mambo ya nje ya Sudan Kusini imetoa taarifa mjini Juba ikisema serikali ya Sudan Kusini imetoa wito kwa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa ufanye uchunguzi wa wazi haraka iwezekanavyo, ili kutafuta chanzo cha ajali na kuchukua hatua ya kuzuia ajali kama hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako