• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yasema mapambano dhidi ya vikundi vya kigaidi vya Turkestan Mashariki yahusishwe kwenye mapambano ya kimataifa ya ugaidi

  (GMT+08:00) 2019-02-12 09:31:10

  Naibu Mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Wu Haitao amesema mapambano dhidi ya vikundi vya kigaidi vya Turkestan Mashariki yanapaswa kuwa sehemu ya mapambano ya kimataifa ya dhidi ya ugaidi.

  Akiongea kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Bw. Wu amesema katika miaka michache iliyopita vikundi vya kigaidi vya Turkestan Mashariki vimepanga na kufanya mashambulizi mengi ya kigaidi katika maeneo mbalimbali ya China. Pia wamekuwa tishio kubwa kwa nchi za Mashariki ya kati na Asia ya kati.

  Amesisitiza kuwa China inapinga ugaidi wa aina yoyote na kusema ikiwa mhusika muhimu wa mapambano ya ugaidi duniani, China imeshiriki kwa kina kwenye ushirikiano wa kimataifa kupitia mifumo na majukwaa kama ya Umoja wa Mataifa na Shrika la Ushirikiano la Shanghai.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako