• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Afisa mwandamizi wa UM aonya juu ya kuridhika na kushindwa kwa kundi la kigaidi la IS

  (GMT+08:00) 2019-02-12 10:24:53

  Afisa mwandamizi wa Ofisi ya Kupambana na Ugaidi ya Umoja wa Mataifa jana alionya nchi mbalimbali juu ya kuridhika kutokana na kushindwa kwa kundi la kigaidi la IS.

  Msaidizi wa katibu mkuu kwenye Ofisi ya Kupambana na Ugaidi ya Umoja wa Mataifa Vladimir Voronkov, ameliambia Baraza la Usalama kuwa licha ya mafanikio ya hivi karibuni dhidi ya IS na washirika wake, tishio linalotokana na magaidi waliorejea na wapiganaji waliohama makazi, pamoja na watu wanaohamasishwa nao, bado ni kubwa na linasambaa duniani.

  Kwa upande wake Naibu Mjumbe wa kudumu wa China kwenye umoja wa mataifa Wu Haitao ametoa wito wa kushirikiana katika kupambana na ugaidi akisema nchi zote zinapaswa kuwa kitu kimoja katika kutumia sera ya kutovumilia kabisa ugaidi.

  Wakati huohuo Jerry Matjila, mwakilishi wa kudumu wa Afrika Kusini kwenye Umoja wa Mataifa amesema Umoja huo bado ni mratibu mkuu katika juhudi za kupambana na vitendo vya ugaidi. Umuhimu wake katika kuunga mkono nchi wanachana katika kukabiliana na changamoto zao za kupambana na IS hauwezi kubezwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako