• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zambia yasema kupiga marufuku mifuko ya plastiki kutatoa fursa kwa biashara mpya

    (GMT+08:00) 2019-02-12 17:07:52

    Mamlaka ya Maendeleo ya Zambia (ZDA) imesema kuwa marufuku ya kutumia mifuko ya plastiki nchini humo itatoa fursa mpya za biashara kwa kutengeneza mifuko inayoweza kutumiwa mara nyingi.

    Mkuu wa Mamlaka hiyo Perry Mapani amesema, sheria hiyo pia inatarajiwa kuchochea uvumbuzi katika sekta ndogo ya ufumaji wa vikapu ambavyo vinakwenda na wakati na vinadumu kwa muda mrefu kwa kutumia vifaa vya kiasili, na hivyo kutoa nafasi zaidi ya ajira.

    Amesema marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki itaanza kutekelezwa tarehe 14 mwezi huu, na pia itasaidia kampuni zinazotumia zaidi ya dola milioni 30 za kimarekani kila mwaka katika kuagiza bidhaa za ufungishaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako