• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yapeleka timu ya wahudumu wa afya mkoa wa mashariki nchini humo

    (GMT+08:00) 2019-02-12 18:45:30

    Uganda imepeleka timu ya wahudumu wa afya katika wilaya ya mashariki ya Tororo baada ya familia moja kupokea maiti ya ndugu yao aliyefariki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwenye mkoa ulioathirika vibaya na mlipuko wa Ebola.

    Msemaji wa wizara ya afya nchini Uganda Emmanuel Ainebyoona amesema, timu hiyo ya wahudumu wa afya tayari imemtambua marehemu na familia, na familia hiyo imewekwa katika eneo maalum kwenye kituo cha afya wilayani humo.

    Amesema cheti cha kifo kinaonyesha kuwa marehemu alifariki kutokana na moyo wake kushindwa kufanya kazi na kifua kikuu, lakini kwa kuwa alikuwa anafanya kazi mashariki mwa DRC, inapaswa kufanya vipimo vyote muhimu ili kuondoa wasiwasi wa maambukizi ya Ebola.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako