• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yazitaka DPRK na Marekani kufanya juhudi ya pamoja ili kufanikisha mkutano wa pili kati ya viongozi wa nchi hizo mbili

    (GMT+08:00) 2019-02-12 18:54:06

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema, China inazitaka Korea Kaskazini na Marekani kujibu ufuatiliaji wa upande mwingine ili kuhimiza kufanyika kwa mkutano wa pili kati ya viongozi wa nchi hizo mbili na kupata mafanikio.

    Mazungumzo kati ya China na Russia kuhusu usalama wa Asia Kaskazini Mashariki yamefanyika hivi karibuni mjini Moscow, na pande mbili hizo zimejadili maendeleo ya hali ya Peninsula ya Korea.

    Bi Hua amesema, pande hizo mbili zinapongeza juhudi za kutatua masuala ya peninsula hiyo kupitia mazungumzo zinazofanywa na Korea Kaskazini na Marekani. Amesema China na Russia zinaunga mkono Korea Kaskazini na Korea Kusini kuboresha uhusiano, kuhimiza ushirikiano na makubaliano, ili kuendelea kufanya juhudi za pamoja kusukuma mbele mchakato wa utatuzi wa kisiasa wa suala la peninsula ya Korea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako