• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Kahawa ya Rwanda yaonjwa China

    (GMT+08:00) 2019-02-12 20:48:05

    Kampuni moja ya china AfriCo, imeandaa hafla ya kuonja kahawa ya Rwanda katika mji wa Xian.

    Rwanda imepeleka bidhaa kumi za kahawa kama vile Gorilla Coffee, Bourbon Coffee, Cafe de Maraba na Three African sisters .

    Halafa hiyo inahudhuriwa na kampuni, watu binafsi na wawakilishi kutoka balozi za Iran, Mauritius, Afrika Kusini, Rwanda, Senegal, Somalia, na Tanzania.

    Mwansilishi wa AfriCo LI Qing,amesema hafla hiyo huangazia mabadilishano ya kitamaduni kati ya China na Afrika na ushirikiano wa kibiashara.

    Mauzo ya kahawa ya Rwanda nchini China yameendelea kuongezeka huku sasa bidhaa hiyo ikipatikna kwenye mtandao wa Alibaba wenye mamilioni ya wateja nchini China.

    Mwaka huu Rwanda inatarajia kupata dola milioni 75 kutoka kwa mauzo ya nje ya kahawa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako