• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mazao safi ya Kenya yanayouzwa nje yaingiza mapato ya dola bilioni 1.53 za Kimarekani

    (GMT+08:00) 2019-02-13 09:10:58

    Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa jana, mapato ya Kenya yanayotokana na mazao safi yanayouzwa nje katika mwaka 2018 yamepanda hadi kufikia shilingi bilioni 153.68 za Kenya ambazo ni sawa na dola bilioni 1.53 za Kimarekani, likiwa ni ongezeko la asilimia 33 kuliko mapato ya mwaka 2017.

    Mkurugenzi wa Shirikisho la Wauzaji nje wa Mazao Safi la Kenya (FPEAK), Hosea Machuki amesema sekta hii imeendelea kufanya vizuri licha ya changamoto mbalimbali kutoka ndani na nje. Amesema usafirishaji wa maua bado unaendelea kuchangia zaidi kwa asilimia 74 ya mapato ya jumla ya mazao safi ambapo mboga na matunda yanaendelea kuchangia kwa asilimia 18 na asilimia 8 mtawalia.

    Machuki amesema Uingereza ndio mnunuzi mkubwa wa mboga ikifuatiwa na Uholanzi na Ufaransa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako