• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa waendelea kutoa msaada wa kibinadamu Syria

    (GMT+08:00) 2019-02-13 09:22:14

    Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw Stephane Dujarric jana alisema wafanyakazi wa kibinadamu kutoka Umoja wa Mataifa wamewapatia msaada watu milioni 2.4 walioko kaskazini magharibi mwa Syria.

    Dujarric amesema msaada wa kibinadamu unaendelea kutolewa kaskazini magharibi mwa Syria, ambako wafanyakazi wa kibinadamu wamechukua hatua ya kupunguza hali ya hatari baada ya mapambano kati ya makundi yenye silaha yasiyo ya kitaifa yaliyotokea mwezi uliopita na kupanua udhibiti wa kundi la Hayat Tahrir al-Sham (HTS). Ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali yanaendelea kuwapatia watu hao vyakula, dawa, mahema, na vitu vingine vinavyohitajika katika majira ya baridi.

    Wakati huo huo, gavana wa mkoa wa Kilis amesema mlipuko wa mabomu yaliyotegwa kwenye gari ulitokea jana kwenye kivuko cha mpakani kati ya Uturuki na Syria, na watu wasiopungua watatu wamejeruhiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako