• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 76 wa Yemen wauawa kutokana na uvunjaji wa makubaliano ya kusimamisha vita Hodeidah

    (GMT+08:00) 2019-02-13 09:22:33

    Waangalizi wa kijeshi wa Hodeidah jana walisema tangu makubaliano ya kusimamisha vita yaanze chini ya usuluhishi wa Umoja wa Mataifa mwezi Desemba mwaka jana, watu 76 wameuawa kwenye kipindi hiki.

    Taarifa iliyotolewa na wasimamizi hao imesema katika kipindi hiki kilichoanzia Disemba 18 mwaka jana hadi Februari 9, waasi wa Houthi wanaodhibiti mji wa bandari Hodeidah ulioko kwenye Bahari Nyekundu wamefanya makosa 1,112 yaliyokiuka makubaliano, ikiwa ni pamoja na matumizi ya silaha dhidi ya makazi ya raia, mahali pa umma na maeneo ya jeshi la taifa mjini Hodeidah, vitendo ambavyo vimesababisha vifo vya watu 76, wengi wao wakiwa ni raia, na wengine 492 kujeruhiwa.

    Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw Stephane Dujarric jana alisema wafanyakazi wa kibinadamu bado hawajaweza kuingia kwenye viwanda vya Bahari Nyekundu vilivyoko mji wa Hodeidah, hali ambayo ameitaja kama "sikitiko kubwa".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako