• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Tanzania haitamsaidia mtuhumiwa wa dawa za kulevya aliyekamatwa nchini Indonesia

    (GMT+08:00) 2019-02-13 09:33:08

    Mamlaka ya udhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya nchini Tanzania DCEA imesema, mtanzania aliyekamatwa mjini Bali, Indonesia kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya asitarajie msaada wowote kutoka serikalini.

    Kamishna mkuu wa DCEA Rodgers Sianga amesema, mtuhumiwa huyo alijua kuwa kitendo alichofanya kinakwenda kinyume na sheria.

    Habari zinasema, mamlaka ya Indonesia imemkamata Abdul Rahman Asman katika uwanja wa ndege akikutwa na kilo moja ya dawa ya kulevya aina ya methamphetamine ndani ya tumbo lake. Bado haijajulikana kama upande wa mashtaka watataka apewe adhabu ya kifo au la, lakini Indonesia ina sheria kali zaidi za dawa za kulevya duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako