• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maelfu ya watu kutoka Sudan Kusini wakimbilia DRC

    (GMT+08:00) 2019-02-13 09:33:25

    Shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limetoa ripoti kuwa, wakimbizi wengi kutoka Sudan Kusini wamekimbilia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

    Msemaji wa UNHCR Babar Baloch amesema, katika siku chache zilizopita wakimbizi wapatao elfu 5 wameingia kwenye vijiji vya mpakani karibu na mji wa Ingbokolo, kaskazini mashariki mwa DRC, wakikimbia mapambano na vurugu dhidi ya raia nchini humo.

    Habari zinasema, raia wengine elfu 8 kutoka viunga vya mji wa Yei wamepoteza makazi yao nchini Sudan Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako