• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IMF yaonya kuwa kiwango cha madeni cha Uganda kitaongezeka hadi kufikia asilimia 49.5 ndani ya miaka miwili

    (GMT+08:00) 2019-02-13 09:44:19

    Shirika la fedha la kimataifa IMF limeonya kuwa kiwango cha madeni ya umma kwa Pato la ndani la taifa GDP nchini Uganda kitaongezeka hadi kufikia asilimia 49.5 ifikapo mwaka wa fedha 2021/22, kutokana na mwendelezo wa matumizi makubwa ya kifedha ya serikali.

    IMF imesema katika miaka mitano iliyopita, bajeti ya Uganda imeendelea kuongezeka na kusababisha ongezeko la matumizi ya umma.

    Kwa mujibu wa wizara ya fedha ya Uganda, madeni ya Uganda yamefikia dola za kimarekani bilioni 10.7, ambayo ni asilimia 41.5 ya pato la taifa. Hata hivyo, serikali ya Uganda imesema kiwango hicho bado ni salama na hakijafikia asilimia 50 ambayo ni mstari mwekundu wa kusababisha msukosuko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako