• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mbunge wa Zambia atoa wito wa kuimarisha zaidi uhusiano kati ya nchi hiyo na China

    (GMT+08:00) 2019-02-13 16:29:05

    Mbunge wa jimbo la Chifubu nchini Zambia Bw. Frank Ng'ambi amesema, nchi hiyo na China zinapaswa kuendelea kuimarisha ushirikiano wa pande mbili ambao umesaidia mageuzi ya uchumi ya Zambia.

    Mbunge huyo amesema, ushirikiano kati ya pande hizo mbili umeleta manufaa ya kiuchumi kwa watu wa Zambia, na kuongeza kuwa China imekuwa rafiki wa muda wote kwa Zambia, ikitoa uungaji mkono kwa miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa reli ya TAZARA.

    Amesema miradi hiyo imeinua kiwango cha maisha ya watu wa huko, na imefanikiwa kuhamisha kwa mafanikio ujuzi na uwezo kwa watu wa Zambia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako