• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuendelea kuunga mkono na kushiriki kwenye operesheni za kulinda amani

    (GMT+08:00) 2019-02-13 18:44:48

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema, China ikiwa moja kati ya nchi kubwa zinazotoa askari na fedha katika operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa, imetoa mchango mkubwa katika kurejesha amani na utulivu wa nchi na sehemu husika na kulinda usalama wa watu na mali zao na kutekeleza majukumu ya kimataifa.

    Habari zinasema, maonesho yenye kaulimbiu ya "Jeshi la China linalolinda amani ya dunia" yamefunguliwa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York. Naibu katibu mkuu wa Umoja huo Bw. Atul Khare amehutubia katika ufunguzi wa maonesho hayo akisema, bila ya uungaji mkono wa nchi wanachama kama China, operesheni hizo haziwezi kupata mafanikio kama ya leo.

    Bibi Hua amesema, China siku zote itaendelea kuunga mkono na kushiriki katika operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako