• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yasema magonjwa yasiyo ya kuambukiza yameyumbisha mfumo wa afya

    (GMT+08:00) 2019-02-14 08:50:52

    Ofisa mwandamizi wa Kenya amesema magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanatishia utulivu wa mfumo wa afya wa Kenya.

    Katibu mkuu msimamizi wa Wizara ya afya ya Kenya Bw. Rashid Amana amesema magonjwa hayo ambayo yameongezeka kwa kiasi kikubwa kutokana na uchafuzi wa mazingira na tabia ya watu kukaa kwa muda mrefu, yamekuwa tishio dhidi ya maendeleo ya Kenya.

    Akiongea kwenye Mkutano wa tisa wa mwaka wa sayansi na afya unaofanyika mjini Nairobi, Bw. Amana amesema magonjwa hayo ni sugu na yamekuwa chanzo cha gharama kubwa za kiafya kwa wakenya.

    Bw. Amana pia amewataka wanasayansi kupanua maeneo ya tafiti zao katika kutambua milipuko ya magonjwa kwa haraka zaidi, kutokana na kuwa Kenya inapakana na nchi ambazo hazina usimamizi imara na mfumo wa afya wenye ufanisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako