• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pompeo na Lavrov wazungumza kuhusu INF na Venezuela

    (GMT+08:00) 2019-02-14 09:03:12

    Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na mwenzake wa Russia Bw. Sergei Lavrov, akisisitiza msimamo wa Marekani kuhusu Mkataba wa Silaha za Nyuklia za Masafa ya Kati INF na suala la Venezuela. Bw. Pompeo amesema Mkataba wa INF unaweza kumalizika mapema Agosti, isipokuwa kama Russia itafuata mkataba huo kikamilifu na kwa njia inayothibitishika. Kuhusu suala la Venezuela Bw.Lavrov amemwonya Pompeo kuwa Russia inapinga Marekani kuingilia kati mambo ya Venezuela ikiwemo matumizi ya kijeshi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako