• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wagombea urais wa Nigeria watoa mwito tena wa kufanyika uchaguzi kwa amani

    (GMT+08:00) 2019-02-14 09:13:10

    Wagombea urais wa Nigeria wametoa mwito tena wa kufanyika kwa uchaguzi mkuu kwa amani, watakapopiga kura kumchagua rais wikiendi hii.

    Jana rais Muhamad Buhari anayetetea kiti kwa tiketi ya chama tawala APC, na mgombea wa upinzani Bw. Abubakar Atiku wa chama cha PDP, walikuwepo mjini Abuja kwenye kusaini "waraka wa amani" ambao ni wa pili kusainiwa tangu Desemba 11, wakiahidi pamoja na vyama vyao kuepuka hotuba za chuki, habari feki na vitendo vyovyote vinavyoweza kuchochea vurugu.

    Akiongea kwenye sherehe ya kusainiwa kwa waraka huo, Rais Muhamad Buhari ameelezwa kuridhishwa na jinsi kampeni zilivyoendeshwa na wagombea wote katika nchi nzima.

    Wagombea wote wamesema watakubaliana na matokeo yatakayotangazwa na tume ya uchaguzi ya Nigeria (INEC).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako