• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini kuwatoza kodi watumishi wa umma kugharamia utekelezaji wa makubaliano ya amani

    (GMT+08:00) 2019-02-14 09:13:33

    Sudan Kusini imesema itawatoza kodi watumishi wa umma ili kugharamia utekelezaji wa makubaliano ya amani yaliyosainiwa mwezi Septemba mwaka jana kati ya pande zinazopambana nchini humo.

    Waziri wa habari wa Sudan Kusini Bw. Michael Makuei Lueth, amesema kwa sasa wanahitaji dola milioni 258 za kimarekani kwa ajili ya utekelezaji wa makubaliano ya amani.

    Bw Makuei pia ameitaka sekta binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali ikiwa ni pamoja na jumuiya ya kimataifa, kuchangia kuunga mkono amani.

    Ofisa wa Kamati ya pamoja ya usimamizi wa amani Bw. Berhanu Kebede, amevikumbusha vyombo vya habari nchini Sudan Kusini kuwa mstari wa mbele katika kujenga amani na kuhimiza masikilizano. Amevitaka vyombo hivyo kutoa habari kuhusu makubaliano yaliyosainiwa na kutoa jukwaa la majadiliano kuhusu makubaliano hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako