• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya watu waliouawa katika shambulizi la kigaidi dhidi ya kikosi cha IRGC cha Iran yafikia 23

    (GMT+08:00) 2019-02-14 09:14:21

    Idadi ya wanausalama waliouawa katika shambulizi la kujitoa muhanga dhidi ya kikosi cha ulinzi wa Jamhuri ya Iran katika jimbo la Sistan na Baluchestan imefikia 23.

    Taarifa iliyotolewa na shirika la habari la ISNA imesema watu 17 walijeruhiwa kwenye shambulizi hilo. Gari lililokuwa limebeba mabomu lililipuka karibu na basi lililokuwa limewabeba wanausalama wa kikosi cha IRGC na kusababisha mauaji na majeruhi hayo.

    Kundi la waasi la Jaish al_Adl limetangaza kuwajibika na shambulizi hilo. Lakini IRGC imesema idara ya ujasusi ya Israel inahusika na shambulizi hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako