• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nigeria yasema takwimu za GDP zinaonesha uchumi wake unakua vizuri

    (GMT+08:00) 2019-02-14 09:27:34

    Serikali ya Nigeria imesema uchumi wa nchi hiyo unakua vizuri, kwani takwimu mpya za pato la taifa GDP zinaonesha kuwa, uchumi unakua kwa kasi zaidi tangu mwaka 2017 ulipoanza kufufuka.

    Takwimu zilizotolewa Jumanne na Idara Kuu ya Takwimu ya Nigeria, pato la taifa la nchi hiyo lilikua kwa asilimia 2.38 katika robo ya nne ya mwaka jana, na kasi hii ni kubwa zaidi tangu uchumi udidimie mwaka 2016.

    Takwimu zinaonesha kuwa kasi ya jumla ya ongezeko la pato la taifa la Nigeria kwa mwaka jana ilikuwa asilimia 1.93, na kuzidi asilimia 0.82 ya mwaka 2016, na ongezeko hilo haswa linatokana na maendeleo ya sekta zisizo za mafuta.

    Katika robo ya pili ya mwaka 2017, uchumi wa Nigeria ulianza kufufuka baada ya kudidimia vibaya tangu miongo miwili iliyopita. Ili kuhimiza maendeleo ya uchumi, serikali ilitekeleza "mpango wa kufufua na kukuza uchumi" wa kuhimiza ukuaji wa sekta zisizo za mafuta.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako