• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNHCR yaipongeza Ethiopia kwa sera yake ya kuwapokea wakimbizi

    (GMT+08:00) 2019-02-14 09:28:19

    Mwenyekiti wa Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR Bw. Philippo Grandi, ameipongeza Ethiopia kwa sera yake ya kufungua mlango kwa wakimbizi kutoka nchi jirani.

    Bw. Grandi ambaye yupo ziarani nchini Ethiopia pia amesifu nchi hiyo kwa kuboresha maisha ya wakimbizi kwa njia mpya na kivumbuzi.

    Takwimu zilizotolewa na UNHCR zinaonesha kuwa, Ethiopia ina zaidi ya wakimbizi laki 9, wengi wao wakitoka Sudan Kusini, Somalia, Sudan na Eritrea, na wachache kutoka Yemen na Syria.

    Kwenye mkutano wa 32 wa kilele wa Umoja wa Afrika uliofanyika hivi karibuni mjini Addis Ababa, viongozi wa Afrika walitangaza mwaka huu kuwa ni mwaka wa wakimbizi, waliorejea kutoka ukimbizini na wakimbizi wa ndani, kwa ajili ya utatuzi wa kudumu wa suala la wakimbizi barani Afrika".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako