• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zimbabwe yaridhia mkataba wa kimataifa wa nyuklia

    (GMT+08:00) 2019-02-14 16:57:34

    Zimbabwe imeridhia Mkataba wa Pande Zote wa Kupinga Majaribio ya Nyuklia, na kuwa nchi ya 168 duniani kuridhia mkataba unaokataza matumizi ya silaha za nyuklia ikiwemo majaribio.

    Akizungumza baada ya kuridhia mkataba huo, rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amesema hatua hiyo ni ishara ya mabadiliko ya nyakati, na kwamba uamuzi huo umefikiwa kutokana na maendeleo mapya nchini humo. Amesema mazingira ya sasa ni tofauti na anaamini kuwa ni sahihi kwa Zimbabwe kuwa upande mmoja na nchi nyingine 167 zilizoridhia kupinga kuenea kwa silaha za nyuklia.

    Mkataba huo uliopitishwa na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa Septemba 10, 1996, unakaribia kupata uaminifu wa kimataifa, huku nchi 184 zikiwa zimesaini na nyingine 168 kuridhia, hata hivyo, mkataba huo bado haujaanza kutekelezwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako