• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Maduro asema Venezuela itafanya juhudi kukuza uwezo wa uzalishaji

    (GMT+08:00) 2019-02-14 18:01:40

    Rais Nicolas Maduro wa Venezuela jana amesema, nchi yake itafanya juhudi kukuza uwezo wa uzalishaji, kujaribu kuwa nchi inayouza vyakula kwa nje, na kutimiza mfumo wa uchumi unaoshirikisha pande mbalimbali.

    Rais Maduro pia amezitaka idara zote za uzalishaji zikusanye nguvu, kuhakikisha utulivu wa ukuzaji wa uchumi, na kukidhi mahitaji wa maisha ya wananchi, na kusisitiza kuwa Venezuela haitashindwa na Marekani, na vitendo vyovyote vinavyojaribu kuharibu utaratibu wa uchumi wa Venezuela vitashindwa.

    Habari nyingine zinasema, mjumbe wa Marekani anayeshughulikia mambo ya Venezuela Bw. Elliott Abrams jana amesema, kwa sasa Marekani haina mpango wa kufanya operesheni ya kijeshi dhidi ya Venezuela. Amesema kutumia nguvu ya kijeshi dhidi ya Venezuela si sera ya Marekani, na kwamba itatafuta njia za kibinadamu, kiuchumi, na kidiplomasia ili kushughulikia mambo yanayohusu Venezuela.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako