• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 20 wahofiwa kufariki katika ajali ya boti nchini Zambia

    (GMT+08:00) 2019-02-14 18:51:40

    Zaidi ya watu 20 wanahofiwa kufariki katika wilaya ya Nchelenge nchini Zambia baada ya boti waliyopanda kupinduka katika Ziwa Mweru jana asubuhi, huku watu wengine 19 wakiokolewa.

    Mkuu wa wilaya hiyo Bw. Derrick Mwelwa amenukuliwa akisema, boti hiyo ilikuwa imebeba abiria 40 pamoja na mizigo, kiasi ambacho kimepitiliza uwezo wa boti hiyo. Amesema upepo mkali katika Ziwa hilo pia huenda umechangia katika ajali hiyo, na kuongeza kuwa boti hiyo ilikuwa haijasajiliwa.

    Uchunguzi wa ajali hiyo bado unaendelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako