• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China haina nia ya kufanya siasa ya kijiografia katika Latin Amerika

    (GMT+08:00) 2019-02-14 19:24:13

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema, tuhuma za Marekani dhidi ya ushirikiano kati ya China na Latin America hazina msingi wowote, na China haina nia ya kufanya siasa ya kijiografia katika Latin Amerika.

    Kauli ya Bi. Hua imekuja baada ya Rais mteule wa El Salvador Bw. Nayib Bukele kuongea na msaidizi wa mambo ya usalama wa taifa wa Marekani Bw. John Bolton kwa njia ya simu, akisema nchi hiyo itakuwa mwenzi mwenye nguvu wa Marekani. Bw. Bolton amesema, pande mbili zimejadili kuimarisha urafiki kati yao na kupambana na vitendo vya uporaji vya China.

    Bi Hua amesema, China na El Salvador zilianzisha uhusiano wa kibalozi juu ya msingi wa kuwepo kwa China moja, unaofuata mwelekeo wa maendeleo ya kihistoria, sheria ya kimataifa, na kanuni za msingi za uhusiano wa kimataifa pamoja na maslahi ya kimsingi ya nchi mbili na watu wao, na haulengi wala kuathiri uhusiano kati ya upande mwingine na nchi nyingine. Amesema China inafurahia Marekani na El Salvador kuendeleza uhusiano juu ya msingi wa kuheshimiana na kutoingiliana. Vivyo hivyo, uhusiano kati ya Marekani na El Salvador hauwezi kuharibu nchi nyingine kudumisha na kuendeleza uhusiano wa kawaida na El Salvador.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako