• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wazalishaji wa sukari Tanzania wasema viwanda vyao bado viko Imara

    (GMT+08:00) 2019-02-14 19:52:26

    Wazalishaji wa sukari wa ndani wamesema si kweli kwamba viwanda vyao vimebweteka kwa kuwa wanaruhusiwa kuagiza sukari nje ya nchi, bali uzalishaji umeongezeka na bado wana nia ya kuongeza zaidi.

    Akizungumza na wadau wa sekta binafsi na wa kilimo juzi, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga alisema Serikali imeamua kusitisha vibali hivyo na badala yake itatumia kampuni nyingine, lengo likiwa ni kuwataka wazalishaji wa ndani kuongeza nguvu ya kuzalisha. Alisema tangu kampuni hizo ziruhusiwe kuingiza sukari, zimeshindwa kuendeleza viwanda vyake ikiwamo hata kulima miwa ya kutosha kwa ajili ya malighafi na badala yake nguvu kubwa imeelekezwa katika kuagiza. Alisema sukari iliyopo ina uwezo wa kuhudumia walaji nchini mpaka Mei na kuanzia Juni, Serikali itaagiza tani 25,000 hadi 28,000 ili kusitokee uhaba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako