• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki zatakiwa kufanya kazi saa 24

    (GMT+08:00) 2019-02-15 20:50:29

    Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw Mrisho Gambo amezitaka Benki kufanya kazi saa ishirini na nne ili kutumia vizuri fursa ya kufungwa maduka ya kubadilisha fedha mkoani humo.

    Maduka zaidi ya 30 ya kubadilisha fedha katika jiji la Arusha yalifungwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) tangu Oktoba 2018, kwa kile kilichoelezwa kukiuka taratibu za biashara.

    Akizungumza wakati akifungua semina ya wafanyabiashara na wajasiriamali wa Mkoa huo iliyoandaliwa na Benki ya CRDB, Gambo amesema tangu kufungwa kwa maduka ya kubadilisha fedha kumekuwa na changamoto kwa watalii kubadilisha fedha.

    Amesema benki ya CRDB ni moja ya benki kubwa nchini Tanzania inayoweza kusaidia kuondoa changamoto hiyo.

    Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema benki hiyo tayari imefungua dirisha maalum ya kubadilisha fedha katika matawi yake yote, ikiwemo kwenye uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (Kia).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako