• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zanzibar : Zanzibar na Oman zaendelea kukuza ushirikiano wao kibiashara

    (GMT+08:00) 2019-02-18 20:17:58

    Mwakilishi wa Kampuni ya Arabian Industries ya Oman, Sheikh Amor Al –Suleimani, amesema Oman inajivunia kuona wawekezaji wa taasisi na kampuni za kibiashara kutoka nchi hiyo, wanashawishika kuongeza kasi ya uwekezaji kwenye miradi ya utalii na uvuvi wa Bahari Kuu.

    Amesema anaamini uwekezaji huo utaongeza mapato na kuimarisha uchumi wa nchi hizo mbili.

    Aliyasema hayo iki alipozungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi.

    Al – Suleimani alimweleza Balozi Iddi kuwa, wananchi wa Zanzibar na Oman hawana sababu ya kutoshirikiana kutokana na uhusiano wao wa kihistoria.

    Alisema uongozi wa Arabian Industries tayari umeshawishika kuwekeza katika miradi ya sekta ya utalii kwa kujenga hoteli ya nyota tano kutokana na fursa za uwekezaji zilizoko visiwani Zanzibar.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako